Shirika la Habari la Hawza - Katika sehemu iliyopita, ilibainishwa kuwa riwaya zinazozungumzia intidhar zimegawanyika makundi mawili, aina ya pili ya riwaya zinahusu kusubiria faraja kwa maana mahsusi, na katika sehemu hii tunazungumzia hilo:
Kusubiria faraja kwa maana mahsusi
Katika maana hii, intidhar ni kusubiri kwa hamu mustakabali wenye sifa zote za jamii ya Kimungu, ambao mfano wake wa pekee ni kipindi cha utawala wa hazina ya mwisho ya Mwenyezi Mungu, yaani kuwepo kwa Mtukufu Wali al-Asr [aj].
Baadhi ya maneno ya Maimamu (a.s) kuhusiana na kusubiria faraja
Imam al-Baqir [a.s], alipokuwa akieleza dini inayompendeza Mwenyezi Mungu, baada ya kutaja mambo kadhaa, alisema:
«...وَالتَّسْلِیمُ لِاَمْرِنا وَالوَرَعُ وَالتَّواضُعُ وَاِنتِظارُ قائِمِنا...»
“…na kujisalimisha kwenye amri zetu, uchamungu, unyenyekevu, na kumsubiri Qā’im wetu…”
(al-Kāfī, juz. ۲, uk. ۲۳)
Imam al-Sādiq [a.s] amesema:
«عَلَیْکُمْ بِالتَّسْلیمِ وَالرَّدِّ اِلینا وَاِنْتظارِ اَمْرِنا وَامْرِکُمْ وَفَرَجِنا وَفَرَجِکُم.»
“Ni juu yenu kujisalimisha na kurejesha mambo kwetu, na kusubiri amri yetu na amri zenu, na faraja yetu na faraja zenu.”
(Rijāl al-Kashī, uk. ۱۳۸)
Maana ya kusubiri
Kutokana na riwaya kuhusiana na kusubiri kudhihiri kwa Imamu Mahdi [a.s], inafahamika kuwa kusubiri kudhihiri kwake sio tu njia ya kuifikia jamii inayotarajiwa, bali subira yenyewe ni ibada na ina thamani, yaani, mtu akiwa katika hali ya kusubiri kwa dhati, iwe atashuhudia kudhihiri au la, bado ana ujira mkubwa.
Mtu mmoja alimuuliza Imam al-Sādiq [a.s]:
«مَا تَقُولُ فِیمَنْ مَاتَ عَلَی هَذَا اَلْأَمْرِ مُنْتَظِراً لَهُ؟»
“Mnasemaje kuhusiana na mtu mwenye kushikamana na wilaya ya viongozi wa kweli, akisubiri kudhihiri kwa utawala wa haki, kisha akafariki katika hali hiyo?”
Imam [a.s] akajibu:
«هُوَ بِمَنزِلَةِ مَنْ کانَ مَعَ القائِمِ فِی فُسطاطِهِ» ثُمَ سَکَتَ هَنیئةً، ثُمَ قالَ: «هُوَ کَمَنْ کانَ مَعَ رُسولِ اللّه.»“Yeye ni sawa na mtu alikuwepo pamoja na Qā’im [a.s] ndani ya kambi yake.”
Kisha alinyamaza kwa muda kidogo, akasema: “Ni kama mtu aliyekuwa pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu [s.a.w.w] katika mapambano yake.”(Bihār al-Anwār, juz. ۵۲, uk. ۱۲۵)
Utafiti huu utaendelea...
Imenukuliwa kutoka katika kitabu kiitwacho Darsnāmeh-ye Mahdaviyyat cha Khodā-Morād Salīmiyān, huku ikifanyiwa mabadiliko kiasi.
Maoni yako